Kocha wa Klabu ya Yanga George Lwandamina raia wa Zambia atamkosa Mchezaji wake Thabani kamusoko baada ya kushindwa kuungana na wenzake katika mazoezi kutokana na kuwa majeruhi.

Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema Kamusoko atalazimika kukosa michezo miwili iliyo mbele yao dhidi ya Kagera na Stand kutokana na majeraha ambayo yatamuweka nje wiki mbili.

Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema Kamusoko atalazimika kukosa michezo miwili iliyo mbele yao dhidi ya Kagera na Stand kutokana na majeraha ambayo yatamuweka nje wiki mbili.

“Kamusoko hayupo katika mpango wa safari ya leo (jana) kutokana na kuumwa kifundo cha mguu ambapo leo ana siku ya nne tangu alipoanza kuumwa, hivyo atalazimika kukaa wiki mbili na kukosa michezo miwili dhidi ya Kagera na Stand’’ amesema Ten.

Hata hivyo, Ten ameongeza kuwa Ngoma atakuwemo safarini lakini mechi dhidi ya Kagera hatacheza, atakuwa anaendelea na matibabu na mazoezi mepesi lakini anatarajiwa kucheza katika mechi ijayo dhidi ya Stand.

Yanga kwa sasa ipo vitani ikiwania kurudi kileleni kutokana na kuwa na pointi tisa hadi sasa ikiwa nafasi ya sita huku wapinzani wao Simba wakiongoza kwa kuwa na pointi 11 sawa na Mtibwa, hivyo kuwa na wachezaji majeruhi ambao ni tegemeo katika kikosi cha kwanza ni pigo na kunaigharimu timu.

Upande wa mashtaka wapewa siku 14
Msemaji wa serikali awataka TUCTA kuacha siasa

Comments

comments