Kaimu Afisa Habari wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Ezekiel Kamwaga amesema hataongeza muda wa kufanya kazi hiyo klabuni hapo, zaidi ya kuheshimu muda wa miezi miwili aliopewa.

Kamwaga ametoa msisitizo huo, alipohojiwa kwenye kipindi cha Hili Game kinachorushwa na Radio Clauds FM mapema hii leo, ambapo amesema hana budi kufanya hivyo kutokana na majukumu yaliyo mbele yake.

“Ninakaimu nafasi ya Afisa Habari kwa muda wa miezi miwili, mwezi ujao nitakuwa naondoka Simba naenda UK, hivyo klabu itamtangaza Afisa Habari mpya. Mchakato unaelekea kukamilika.” Amesema Kamwaga.

Kuhusu Mabadiliko anayoyaona Simba SC, baada ya kurejea katika kitengo cha habari, Kamwaga amesema kuna mabadiliko makubwa ya kiutendaji pamoja na watu wazito wanaounda Bodi ya Wakurugenzi chini ya Mohamed Dewji ‘Mo’.

“Simba ni ile ile, mashabiki ni wale wale niliowaacha 2013, kilichobadilika sana Simba, imeanza kuwa klabu yenye watu wenye heshima zao, sasa hivi kuna watu kama akina Dr Janabi, akina Mo Dewji, Barbara. Lakini pia sasa kuna mabadiliko kwenye social media.”

Kamwaga alitangazwa kuwa Kaimu Afisa Habari wa Simba SC, baada ya klabu hiyo kuamua kuachana na Haji Manara mwishoni mwa mwezi uliopita, kufuatia tafrani iliyojitokeza kati yake na Uongozi wa klabu hiyo.

Kamwaga adokeza Tamasha la Simba Day 2021
Bocco aachwa Dar es salaam