Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege ameagiza kuvunjwa kwa Mkataba wa Tsh. Bil 3.2 kwa ajili ya Ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Butiama iliyokuwa ikijengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

Ameyasema hayo kufuatia Ukaguzi alioufanya baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ziara yake Mkoani Mara na kumuagiza kufanya  Ukaguzi huo kutokana na kutoridhishwa na taarifa aliyoipokea kutoka kwa Meneja wa TBA.

Amesema kuwa katika ukaguzi wake amebaini kuwepo kwa kasi ndogo ya utekelezaji wa Mradi huo na kubadilishwa kwa eneo lililofanyiwa usanifu hapo awali kwa ajili ya ujenzi badala yake kazi hiyo kufanyika katika eneo tofauti na lile la awali hivyo kuiongezea Serikali gharama ya Tsh Mil. 180.

Aidha, ameongeza kuwa taarifa iliyotolewa na Meneja wa Wakala wa Majengo Mkoa wa Mara kwa Waziri Mkuu ilieleza kuwa kati ya Tsh. mil. 600 zilizopokelewa Aprili, 2017 kutoka Serikali kuu, Tsh Mil. 400 zimekwishatumika kujenga msingi na kazi hiyo imekamilika kwa asilimia 60 tofauti na hali aliyoikuta alipotembelea  eneo hilo la Mradi.

‘Kwa kuzingatia makosa hayo yote Serikali inaagiza kuvunjwa kwa Mkataba wa ujenzi wa Ofisi za Halmashauri uliokuwa utekelezwe na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kushindwa kutekeleza mradi huu kwa wakati, kuongeza gharama za mradi kinyume cha taratibu bila kupata kibali cha Baraza la Madiwani na Ofisi ya Rais TAMISEMI sambamba na kutoa taarifa za uongo kwa Waziri Mkuu,” Amesema Kandege.

 

Chadema yamgeuzia kibao Mkuu wa Wilaya
Video: Aslay na Nandy waiibua bongo fleva kivingine ''Subalkheri Mpenzi''