Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Kangi Lugola amenza ziara ya kikazi ya siku saba katika Jiji la Dodoma kwa lengo la kukagua utekelezaji na uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira nchini.

Lugola ametembelea Ofisi za Jiji na kupokea taarifa ya hali ya mazingira katika usimamizi wa Taka ngumu, taka za maji pamoja na madini ujenzi.

Akitoa taarifa ya Jiji Mkurugenzi, Godwin Kunambi amesema kuwa Ofisi yake imepanga kujenga mabwawa makubwa ya maji taka katika eneo la Nzuguni na ujenzi wake uko mbioni kuanza.

Aidha, katika hatua nyingine, Lugola ameuagiza uongozi wa Hospitali ya Dodoma kuhakikisha changamoto hiyo ya mtambo wakuteketeza taka unapatiwa ufumbuzi mapema ili kuhifadhi mazingira.

Pia ametoa muda miezi nane kwa uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha mfumo wa matumizi ya kuni kama nishati ya kupikia unasitishwa na kuwataka watumie gesi ili kuhifadhi mazingira.

Hata hivyo, ziara ya Naibu Waziri huyo inaendelea kwa kutembelea machinjio ya Punda Kizota na Machimbo ya Mchanga na Kokoto – Chogongwe.

 

Wanafunzi wadondoka dondoka na kutetemeka shuleni
Wanafunzi wakumbwa na tatizo la kudondo dondoka