Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepongezwa kwa hatua yake ya kuwatetea baadhi ya watuhumiwa ambao wamekuwa hawatendewi haki pindi wanapokuwa mikononi mwa jeshi la polisi.

Hayo yamesemwa Jijinji Dar es salaam Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na Mtandao wa Kutetea Haki za Binadamu (THRDC) na kutangaza kuanzishwa kwa operesheni maalum iliyopewa jina la “Tetea haki za Watuhumiwa” lengo ni kuwatetea watuhumiwa wa makosa mbalimbali.

“Tunampongeza Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kujitokeza kuwatetea baadhi ya watuhumiwa nchini, kwa mujibu wa sheria jeshi la polisi lina wajibu wa kumpa mtuhumiwa haki yake ya kupata msaada wa kisheria kitu ambacho kwa Loliondo imekuwa shida na hii ni kwa maeneo yote ya vijijini siyo Loliondo pekee”, amesema mratibu wa mtandao wa THRDC Onesmo Olengurumo.

Hata hivyo, mara kwa mara, Kangi Lugola amekuwa akiwachukulia hatua baadhi ya Makamanda wa Polisi ambao wamekuwa hawatoi haki kwa watuhumiwa wa matukio mbalimbali ya kihalifu.

Muleba yajipanga kukusanya mapato kwa 100%
Mauaji ya watoto tishio mjini Njombe, wananchi waiangukia serikali