Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemtaka Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Bunda kuwakamata watu walioshiriki kuwatapeli wananchi katika Sekta ya michezo wilayani humo, mkoani Mara.

Ametoa agizo hilo wakati akizungumza wananchi wa Mji wa Bunda baada ya kuzindua Bonanza la Amani wilayani humo, amesema kuwa kitendo walichokifanya watu hao ni ufiadi mkubwa hivyo lazima wakamatwe ili iwe funzo kwa wale wote wenye tabia ya kufanya ufisadi wa aina hiyo katika sekta ya michezo nchini.

“Nimeambiwa wanamichezo ambao walichangishwa waliandamana mpaka kwa Mkuu wa Wilaya kuelezea jinsi walivyoibiwa na watu hao, hata hivyo Mkuu wa Wilaya aliwataka watu hao warudishe fedha hizo, ila mimi nahitaji hawa watu wakamatwe haraka iwezekanavyo, huu ni ufisadi mkubwa na hakika Serikali hii ya awamu ya nne haitakubaliana na ufisadi huo,”amesema Kangi Lugola

Aidha, ameongeza kuwa mahakama ya mafisadi inahitaji wateja hivyo waliofanya wizi huo pia ni mafisadi hivyo lazima wakamatwe haraka iwezekanavyo ili sheria ichukue mkondo wake.

Hata hivyo, Bonanza ambalo alilizindua waziri huyo, linatarajiwa kufanyika nchi nzima limezinduliwa mjini humo na baadaye litafanyika nchi nzima likiwa na lengo la kutangaza amani nchini.

 

Lema atembezewa kichapo, wawili wachomwa kisu Arusha
Habari Picha: Wananchi waendelea kupiga kura jimbo la Buyungu mkoani Kigoma