Mbunge wa Mwibara, Kange Lugola (CCM) ameeleza mtazamo wake kuhusu kauli ya Rais John Magufuli aliyoitoa hivi karibuni katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kuhusu wanafunzi zaidi ya 7000 wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) waliorudishwa nyumbani.

Akiongea na waandishi wa habari mjini Dodoma, mbunge huyo alieleza kuwa anaamini wasaidizi wa Rais Magufuli hawampi taarifa za kweli.

“Hata siku ile wakati natoa mchango wako kwa Wizara ya Elimu, nilisema kwamba Mheshimiwa Rais ambaye analitumikia Taifa hili kwa nia njema, watendaji wake wanampotosha,” alisema.

“Wanamueleza vitu ambavyo ni tofauti. Wale walioondolewa pale UDOM… narudia tena walikuwa hawasomi degree (shahada), walikuwa wanasoma Diploma (stashahada). Na hata mimi ningekuwa ni mtu wa ajabu sana kuona mwanafunzi amabye amemaliza tu kidato cha nne halafu akaenda kusoma chuo kikuu [degree],” aliongeza.

Kauli ya Lugola imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Rais John Magufuli kueleza kuwa baadhi ya wanafunzi wa UDOM waliorudishwa nyumbani hivi karibuni hawakuwa na sifa za kusoma degree kwakuwa walitumia vyeti vya kidato cha nne wakiwa na daraja la nne.

“Ukimchukua mtoto wa form four ukampeleka pale, hata kama atafanikiwa kupata Degree… itakuwa ya ajabu,” alisema Rais Magufuli.

Alisema kuwa Serikali itawatayarishia mazingira mazuri wanafunzi wenye sifa ili waendelee na masomo yao lakini wale wasio na sifa wakatafute vyuo vinavyoendana na sifa walizonazo.

 

Hatari: Mrembo anyonyoka nywele kwa Kusuka ‘Weave kichwani’
Habari Mpasuko: Muhammad Ali afariki