Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha limewataka maharusi wanaojitambua kuwa sio mabikira ikiwa ni pamoja na wajawazito kutovaa shela.

Askofu mkuu wa kanisa wa Jimbo hilo, Issack Amani, ametoa muongozo huo wa kanisa kwa waumini, tamko ambalo limesisitizwa wiki hii na Paroko Msaidizi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Theresa, Padre Festus Mangwangi.

Padre Mangwangi amesema kuwa kanisa hilo halitafungisha ndoa kwa maharusi wenye ujauzito ambao watafika altareni wakiwa wamevaa shela.

Amesema kuwa wakati wa mafundisho ya ndoa, makatekista watawasisitizia maharusi kuhusu muongozo huo wa kanisa kwa kutovaa shela kama wanajitambua kuwa ni wajawazito au sio mabikira.

Alisema ingawa hakuna vipimo, kwa wanaojitambua kuwa wanamjua mume tayari (sio bikira) lakini wakavaa shela wakatuwa wanafanya udanganyifu mbele ya Mungu. Padre huyo alisema kuwa wanaoweza kudanganya hasa ni wale ambao ujauzito wao unakuwa mdogo.

“Wanaojitambua kuwa sio bikira, hawavai shela, lakini wako wanaojificha na kuvaa shela, hii ni inakuwa sawa na kudanganya,” Padre Mangwangi anakaririwa.

Kiongozi huyo wa kidini aliwataka wazazi kuanza kuwafunza watoto wao kujitambua na kutunza miili yao ambayo ni hekalu la Mungu hadi watakapofunga ndoa.

 

Aliyemchoma kisu mdogo wa Heche apandishwa kizimbani
Video: Kanisa lazuia shela maharusi wajawazito, Familia ya kina Heche yagomea rambirambi

Comments

comments