Waumini wa kanisa la Jubilee Christian Church (JCC) huko nchini Kenya wamejikuta wakigawanyika makundi mawili mara baada ya askofu wao kutaja ujio wa mgeni ulioleta utata na gumzo kubwa miongoni mwa wauamini hao.

Mgawanyiko huo ulitokea mara baada ya Askofu Allan na mchungaji Kathy Kiuna kumkaribisha mwandishi wa habari kutoka CNN, Richard Quest aliyefunguka na kuweka wazi kuwa ni shoga.

Mualiko huo waliutangazwa kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter ukidai kuwa mwanahabari huyo atajumuika pamoja na waumini wa JCC katika misa ya jumapili ijayo.

Wapo waliosema kitendo cha kumkaribisha shoga huyo kanisani ni sawa na kuunga mkono biashara ya ushoga inayofanywa na mwandishi huyo, lakini pia wapo walisema tunaishi katika dunia huru hivyo haitakiwi kuhukumiana.

Quest kwa mara ya kwanza alifunguka juu ya kuwa shoga mwaka 2014, na kusema kuwa yeye kuwa shoga haiathiri biashara na kazi yake ya uandishi wa habari.

Alipofanyiwa mahojiano na kituo cha radio cha Capital FM jana asubuhi alipinga vikali kitendo cha wakenya kuwachukulia tofauti watu wenye mapenzi ya jinsia moja na kusema watu hao wanapaswa kufanya shughuli zao wakiwa huru.

Ameongezea kuwa ili Kenya iwe nchi yenye maendeleo inabidi iwaache watu waishi watakavyo na kuwapenda kwa vile walivyochagua kuwa na kwa kile wanachotaka kukifanya.

Hata hivyo nchi zote za Africa zinapinga vikali ikiwa ni pamoja na kutounga mkono harakati za mapenzi ya jinsia moja.

 

Ukeketaji wahamia kwa vichanga
Mashabiki 60,000 kushuhudia Al Ahy Vs Esperance