Kanisa la Good News for All Ministry limefanya maombi ya kuwaombea viongozi wa kitaifa ili watekeleze majukumu yao bila vikwazo.

Maombi hayo yamefanyika katika eneo la Mapinga Wilaya ya Bagamoyo na yaliongozwa na Mwenyekiti wa Good News for All Ministry, Askofu Dk. Charles Gadi, amesema kuwa maombi hayo ni mwitikio wa kumuombea Rais Magufuli na wasaidizi wake afya njema.

“Maombi haya tumeanza tangu Julai mwaka jana na tunayafanya kila jumanne, tunaendelea nayo katika Mikoa mbalimbali hapa nchini kwa kushirikiana na dini na madhehebu mbalimbali,”amesema Gadi.

Aidha, amesema kuwa wanaamini kwamba katika maombi hayo, nchi itaendelea kusonga mbele kiuchumi na kugundua zaidi maeneo mengine yenye Gesi,Mafuta na Madini,ambayo yatazidi kuukuza uchumi wa nchi katika kujiletea maendeleo.

Mpinga: Hakuna trafiki anayelipwa kukamata magari
Wakurungenzi wengine Tanesco watumbuliwa