Kanisa moja nchini Afrika Kusini linalojulikana kwa jina la Gabola limekuwa likibatiza waumini wake kwa kutumia pombe ili waweze kuwa wafuasi wa kanisa hilo.

Katika kipindi cha maombolezo ya mwanaharakati aliyepigania uhuru wa Afrika Kusini, ‘Winnie Mandela’ kundi la waumini wa dini hiyo walijitokeza wakiwa wamelewa huku wakilia na kudai kuwa ni haki ya kufanya hivyo.

Aidha, mwasisi wa kanisa hilo Father, Tsietsi D Makiti, 53 kwa sasa anajiita Papa wa kwanza mweusi kutoka barani Afrika.

“Mnasema kuwa pombe husababisha vita, ajali, watu kupigana nyumbani na uzinzi, si kweli hata kidogo. mambo haya yote huwatokea hata watu wasiokunywa pombe, wapita njia hugongwa na magari, baadhi ya madereva huwa si walevi, watu kupigana na mizozo mingine hivi vyote vipo hata katika makanisa yasiyotumia pombe,”amesema Father Makiti

Kwa mujibu wa Katiba ya Afrika Kusini inasema kuwa kila mtu ana haki ya kuabudu anavyotaka na ndio maana kila kukicha nchini Afrika Kusini kunaibuka makanisa mapya kama uyoga.

Hata hivyo, Ili kuwa mwanachama kamili wa kanisa hilo lazima Papa Makiti akubatize kwa pombe unayoipenda zaidi, inaweza kuwa Johnnie Walker Red Label, Guinness, Smirnoff na kama ingekuwa Afrika Mashariki pengine Serengeti, Castle, Tusker au hata Konyagi.

 

 

 

 

Aliyemuua mhadhiri UDOM ashikiliwa na polisi
Chidi Benz atiwa mbaroni tena