Serikali ya Botswana huko mjini Goborone, imethibitisha kulifungia  kanisa la Christian Gathering Church la muhubiri Bushiri ambaye ni raia wa Malawi anayedaiwa kutembea hewani.

Serikali ya Botswana imetangaza kuwa kanisa hilo litafungwa kabisa, huku gazeti la Botwana limepokea barua inayoeleza kuwa kibali cha kanisa hilo kimefutwa kutokana na kutumia ‘fedha za miujiza’ ambapo ni kuvunja sheria za Taifa hilo.

Katika mtandao maarufu nchini Malawi wa Malawi24 imetoa ripoti kuwa kanisa hilo lilipinga uamuzi wa kufungiwa Mahakamani mwaka mmoja baada ya muhubiri huyo kupigwa marufuku kuingia nchini humo.

Bushiri ambaye ana zaidi ya ”likes” milioni 2.3 katika mtandao wa facebook na ambaye alivutia umati mkubwa wa kuweza kujaza uwanja wa FNB mkesha wa mwaka mpya bado hajatoa tamko lolote.

Umaarufu wa kanisa hilo ni kutokana na mtindo wake wa maisha ya kifahari ambao umevutia wafuasi wengi barani Afrika.

Hata hivyo Mchungaji Bushiri amewahi kushutumiwa kwa kosa la kuwatoza waumini wake lkiasi kikukbwa cha pesa kati ya dola 80 hadi 2000 waliotaka kula naye chakula cha jioni.

Video: Kibao kipya cha Barnaba ft Aslay ''Ngoma''
Lowassa uso kwa uso na Mbowe, amueleza kilichojiri Ikulu