Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amekutana na Rais wa Marekani, Donald Trump Ikulu jijini Washington kwa ajili ya mkutano wa siku moja wa kuboresha ushirikiano wao katika maeneo mbalimbali ya kiuchumi na kijeshi.

Ziara za mfululizo za viongozi hao zinasemekana kuwa zina lengo la kumshawishi Rais Trump kutotupilia mbali makubaliano ya nyuklia ya Iran na kuondoa ushuru wa kudumu kwa vyuma na aluminium kwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Aidha, imeripotiwa kuwa wakati wa mkutano wao mwezi Machi 2017, viongozi hao hawakupeana mikono wala kuzungumza chochote mpaka walipowasiliana kwa njia ya simu.

Hata hivyo, Angela Merkel anasifika kwa msimamo wake wa kusimamia kipaumbele chake cha misingi, maadili pamoja na maslahi ya pande zote.

Rick Ross kutumbuiza Kenya leo
Nimesikitishwa sana na kitendo cha polisi- Ridhiwani

Comments

comments