Mchekeshaji wa Uganda, Malkia wa burudani ya vichekesho, Kansiime Kubiryaba Anne maarufu kama  Anne Kansiimene,  mwishoni mwa mwaka 2014,aliweza kujiendeleza kiuchumi kwa kuamua kufungua baa na mgahawa uitwao Kubby’s Bar and Restaurant maeneo ya Naalya.

January mwaka huu, amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya watu wasiojulikana kuvamia kwenye baa yake na kupora mali.

Watu hao walivamia kwenye baa hiyo na kuchukua pesa pamoja na mali ikiwemo viti, televisheni, na vinywaji.

Licha ya kupigwa na butwaa, Kansiime amesema anaamini atawapata wezi hao.

Inadaiwa kuwa nyota huyu anawasiwasi na wachekeshaji  wenzake huenda wakawa wanahusika moja kwa moja na tukio la uvamizi huo.

 

 

Walia na Bodi ya mikopo kuwakata 15%
Kinara wa madawa ya kulevya 'EL Chapo' apandishwa kizimbani