Kiungo wa Chelsea N’golo Kante amesita kuhudhuria mazoezi ya klabu yake katika siku ya pili kwa kile kinachoelezwa kwamba Kante bado ana hofu na jinsi idadi ya vifo inavyoongezeka nchini England.

Takwimu kutoka serikalini zinasema watu wenye asili ya ngozi nyeusi wanaongoza kwa vifo hivyo kupelekea wachezaji wengi wenye ngozi nyeusi kusita kuanza mazoezi ya pamoja.

Chelsea walianza mazoezi Jumanne na Kante alikua mmoja kati ya waliohudhuria lakini juzi Jumatano akasita kuhudhuria huku kocha wake Frank Lampard akisema hatamlazimisha mchezaji yeyote kufanya mazoezi kama bado ana hofu.

Tayari vilabu vingi vya ligi kuu ya England wameanza mazoezi huku wakifata miongozo ya wizara ya afya jinsi ya kujilinda na maambukizi na huenda tukashuhudia ligi hiyo ikirejea mwezi ujao.

Mitihani ya Kidato cha sita kuanza rasmi juni 29
Watanzania 119 warejea nchini kutoka Falme za Kiarabu

Comments

comments