Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametoa siku 30 kwa mkandarasi wa SUMA JKT, aliyepewa kazi ya kujenga jengo la ofisi ya wizara hiyo katika mji wa serikali eneo la Ihumwa, Jijini Dodoma.
 
Amemtaka Mkandarasi huyo kufanya kazi usiku na mchana ili aweze kukamilisha ujenzi wa jengo hilo ndani ya siku hizo 30.
 
Ameyasema hayo mara baada ya kutembelea eneo hilo la ujenzi wa jengo la ofisi za Wizara hiyo linalotarajiwa kugharimu shilingi bilioni moja za kitanzania katika eneo la Ihumwa jijini Dodoma.
 
Aidha, Kanyasu amemtaka mkandarasi huyo wa SUMA JKT kuhakikisha anajenga jengo hilo kwa umakini, umahiri na viwango vya ubora wa hali ya juu vinavyokwenda sambamba na hadhi ya wizara yenye mchango mkubwa kwenye pato la Taifa.
 
Ameielekeza SUMA JKT wakati ikiendelea na maandalizi ya ujenzi wa jengo iwe inatoa taarifa kila siku kwa kila hatua inayofikia katika Ujenzi wa jengo hilo kwa Uongozi wa Wizara.
 
Awali, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Lusius Mwenda amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa eneo hilo litakalojengwa Ofisi za Wizara hiyo lina ukubwa wa Hekta 2. 27
 
  • JPM amjulia hali Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi
  • Serikali yatangaza neema ya dawa hospitalini
  • Msinililie mimi bali daini tume huru ya uchaguzi- Mbowe
 
Hata hivyo, eneo la Ihumwa katika Mji wa Dodoma ni eneo rasmi ambalo limetengwa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya serikali yakiwemo ya wizara ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ofisi za serikali kuhamia rasmi jijini Dodoma, kutokana na agizo lililotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wakati akiingia madarakani mwezi Novemba 2015

Hatma ya Diane Rwigara na familia yake kufahamika
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 6, 2018