Kanye West anadaiwa umuajiri mpiga picha kwa ajili ya kumpiga picha yeye na mwanamke anayedaiwa kuwa mpenzi wake mpya Julia Fox, katika hali inayodaiwa kuwa jaribio la kumfanya Kim Kardashian apatwe na wivu ambao utakaompelekea kumrejea Kanye.

Kwa mujibu wa mtandao wa RadarOnline ni kuwa Kanye aliwalipa wapiga picha, jana usiku walipoonekana wakijivinjari na Julia ili kumpa wivu Kim.

Siku za hivi karibuni Kanye West ameonekana akiwa na wanawake wengi tofauti tofauti, lakini mashabiki wameanza kuamini kuwa yeye na mrembo Julia Fox wanaweza kuwa kwenye uhusiano.

Hapo awali alionekana akiwa na Julia wakila chakula cha jioni katika mgahawa mmoja uliopo Carbone huko Miami. Picha kadhaa zilienea mitandaoni zikiwaonyesha wawili hao wakifika mahali hapo na pia wakiwa kwenye meza ya chakula wakitazamana machoni.

Sio Kanye West  pekee ambaye anavishikilia vichwa vya habari, aliyekuwa mkewe pia mrembo Kim Kardashian naye amekuwa akitajwa kwenye habari mbali mbali kila kukicha akizungumzwa juu ya uhusiano wake na mchekeshaji Pete Davidson.

Kwa mujibu wa TMZ, ni kweli kwamba siku za hivi karibuni Kim na Pete walichukua ‘baecation’ kidogo huko Bahamas, jambo lililozalisha taswira ya kuwa ni kweli mrembo huyo pengine amekubali kumsahau Kanye westi moka kwa moja.

Wakati huo huo Kanye West ameripotiwa kuibomoa nyumba yake mpya aliyoinunua kando na mahali anapoishi Kim na kuanza ujenzi wa haraka kwa kuwa anahitaji kuyafanya makazi yake, ili kuwa karibu na mama watoto wake Kim Kardashian.

Mipango ya Kanye na namna anavyotekeleza mambo yake bado ni kitendawili kwa mamilioni ya mashabiki wake ulimwenguni huku maswali yakiwa Je, hatma yake itakuwaje??

Gwajima: Spika Ndugai ajiuzulu, kuna nia ovu
Shiboub kumng'oa Wawa Simba SC