Rapa maarufu nchini Marekani, Kanye West ambaye kwa sasa anataka aitwe ‘YE’ amempa zawadi ya kiatu aina ya snika raisi wa Uganda, Yoweri Museveni alipokutana naye Ikulu katika ziara yake nchini humo.

Rais Museveni amefurahia zawadi hiyo kwa kuandika ujumbe katika akaunti yake ya Twitter kuwa amefurahia snika nyeupe alizopewa na rapa Kanye West kama zawadi, pia amesisitiza ujio wa msanii huyo nchini humo utasaidia kutangaza sekta ya utalii ya nchi hiyo.

Drake afichua alivyotaka kumuoa Rihanna
Somalia yaadhimisha siku ya 'Black Day'

Comments

comments