Mitandao ya kijamii imeongeza ukubwa wa dunia, na hivi sasa ni sehemu inayochangia migogoro mingi kwenye maisha ya binadamu, kama ilivyochangia moto kwenye tanuru la ugomvi wa Kanye West na Drake kuhusu Kim Kardashian.

Leo, Kanye West ameonesha kughafirika baada ya kubaini kuwa Drake alimfuata mkewe Kim Kardashian kwenye Instagram tangu Septemba mwaka huu wakati ambapo tayari kulikuwa na bifu kati yao.

Rapa huyo wa ‘Heartless’ ameaandika na baadaye kufuta ujumbe uliosomeka, “Sikuwahi kufahamu hadi hii leo asubuhi kuwa Drake anamfollow mke wangu Instagram tangu Septemba.”

“Imenibidi nilianike hili suala hapa kwa sababu ni kitu kibaya kuliko vyote na nimekiona leo asubuhi,” aliongeza kwenye maelezo yake.

Kanye na Drake wamekuwa kwenye bifu zito mwaka huu hasa baada ya rapa huyo mzaliwa wa Canada kudaiwa kueleza kuwa amewahi kuwa na uhusiano na Kim Kardashian wakati akiwa na Kanye.

Tetesi hizo ziliibuka zaidi baada ya Drake kuachia wimbo wa ‘In My Feeling’ ambao anamuimbia ‘Kiki’ ambalo ni jina lingine la Kim Kardashian.

Katika mfululizo wa maandishi ya Kanye West leo, aliandika pia ujumbe, “hebu pata picha una matatizo na mtu fulani halafu anamfuata mkeo kwenye Instagram. Tunamtakia kila la kheri mtu huyu na tunamuombea apate furaha ambayo tunaipata sisi. Mpende kila mmoja.”

Liverpool yaipasua Arsenal, Firmino achoma kibanda cha bunduki
HapoKale: Wachaga na kisa cha kurudi nyumbani kila mwisho wa mwaka