Rapa Kanye West ameamua kujirudi na kuwaomba radhi watu aliowakwaza kufuatia kauli yake kuhusu suala la utumwa wa Afrika aliyoitoa mwanzoni mwa mwaka huu.

Kanye alitumia nafasi ya mahojiano aliyokuwa anafanya na kituo kimoja cha redio cha Chicago wiki hii kueleza kwa hisia jinsi ambavyo ameumizwa na kauli yake na kufikia hatua ya kumwaga machozi.

“Sifahamu kama niliwahi kuomba radhi vizuri kwa kauli yangu kuhusu suala la utumwa na nilivyowafanya watu wajisikie vibaya,” alisema Kanye West.

“Ninamba radhi kwa madhara niliyoyasababisha kupitia kauli yangu hiyo kuhusu utumwa, na ninawaomba radhi watu wote walioumizwa wakati huo,” aliongeza.

Aliendelea kutoa shukurani kwa vyombo vya habari kwa kumpa nafasi ya kuzungumzia suala hilo na kueleza kuwa wamempokea na kumtendea mema kama familia.

Aliahidi kuwapa mashabiki wake wa Chicago kitu tofauti kwakuwa amejirekebisha na kwamba wataenda kupata ladha ya Kanye West mpya.

Bosi huyo wa lebo ya Good Music alijikuta matatani baada ya kufanya mahojiano na TMZ na kueleza kuwa anachoamini ni kwamba Waafrika kuingia utumwani lilikuwa “ni chaguo lao”.

Video: Magufuli amshushia nyundo Makonda, Dk. Bashiru atema nyongo
Trump atishia kuing'oa Marekani WTO

Comments

comments