Rapa kutoka nchini Marekani, Kanye West, amenaswa akiwa na mwanamke mwingine licha ya kusikika akilipambania penzi lake na aliyekuwa mke wake, Mwanamitindo maarufu Kim Kardashian.

Kanye alipambana kiasi cha kuamua kununua nyumba mpya kando ya eneo analoishi Kim ili tu kuwa karibu naye.

Habari mpya kumuhusu Kanye West zimeibua mkanganyiko mara baada ya rapa huyo kuonekana akiwa na muigizaji maarufu Julia Fox.

Wawili hao walionekana kwenye mgahawa wa hadhi ya juu huko Miami wakistarehe huku wakionekana kuwa wenye furaha.

Kwa mujibu wa PageSix, chanzo cha karibu kilisema siku hiyo “haikuwa mbaya,” na kwamba Kanye anajaribu kujifurahisha wakati wa sakata la talaka yake linaloendelea baada ya Kim kuomba waachane kisheria.

Harakati hizi za Kanye kujaribu kumsahau Kim inaingia kwenye orodha ya majaribio takribani matatu aliyowahi kuyafanya rapa huyo ili kujaribu kumsahau Kim Kardashian.

Taarifa rasmi za talaka ya Kim na Kanye ziliibuka kwa mara ya kwanza Februari 2021.

Kim na Kanye walifunga ndoa yao rasmi mwaka 2014 wakiwa wamebarikiwa kupata watoto wanne, binti North mwenye umri wa miaka 7, mtoto wa kiume aitwaye Saint (5), binti aitwaye Chicago(3), pamoja na Psalm, 2.

Rais Mwinyi atengua uteuzi wa Mkurugenzi ZBC
Shiboub, Tenana kukiwasha Mapinduzi CUP 2022