Rapa Kanye West ametangaza njaa kwa mashabiki wake muda mfupi kabla ya kupanda jukwaani Jumamosi iliyopita akiwaomba wamsaidie kumaliza tatizo la mikopo inayomkabili.

Rapa huyo aliandika tweet kadhaa akieleza kuwa anakabiliwa na madeni yenye kiasi cha $53 milioni ambazo zinampasua kichwa.

I write this to you my brothers while still 53 million dollars in personal debt… Please pray we overcome… This is my true heart...,” inasomeka tweet ya ya kwanza ya Kanye West.

Baadae aliwataka mashabiki wake kujiunga na Tidal wanunue albam yake mpya ya ‘The Life of Pablo’, ikiwa ni hatua ya kumsaidia kupata fedha za kulipa madeni yake.

Inaonekana watu walikuwa na mwitikio chanya kwa ombi lake, kwani baada ya saa chache, mtandao wa Tidal unaomilikiwa na swaiba wake Jay Z, ulishika nafasi ya kwanza App Store zote za iOS ikiwa ni mara ya kwanza kwa mtandao huo kushika nafasi hiyo.

Albam mpya ya Kanye imeonekana kumpasua kichwa kiasi cha kubadili jina mara kadhaa ili kuwaweka sawa mashabiki wake. Hivi sasa Kanye anadai kuwa ‘The Life of Pablo’, maaana yake ni maisha ya Mtume Paulo.

Mrema: Magufuli anatenda miujiza
ACT Wazalendo walia na Magufuli, Wakosoa jitihada za mabadiliko ya Mfumo