Rapa Kanye West, amefunguka kuwa yuko mbioni  kuiachia albamu yake inayofuata, ambayo ni muendelezo wa ‘Donda’ ya mwaka jana itakayotoka mapema mwezi ujao.

Alhamisi hii Januari 27, 2022, Ye ametangaza rasmi kuwa ‘Donda 2’ ataiingiza sokoni rasmi ifikapo Februari 22, 2022.

Kanye ametoa taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram huku akibainisha kuwa, ‘future’ ndio mtayarishaji wa Album hiyo ‘Donda 2’.

Donda ya awali iliachiwa rasmi mnamo Agosti 29, 2021, ni album iliyopewa jina la marehemu mama mzazi wa rapa Kanye West, ambayo imefanikiwa kufanya vizuri kiasi cha kutajwa kwenye vipengele kadhaa vya tuzo za Grammy.

Ikiwa ni pamoja na albamu bora ya mwaka na albamu ya rap ya mwaka, wimbo ‘Hurricane’ aliyowashirikisha The weekend na Lil Baby, pamoja na ‘Jail’ aliyomshirikisha Jay-Z, zimetajwa kwenye vipengele tofauti tofauti vya tuzo hizo kubwa ulimwenguni.

Chris Brown ashitakiwa kwa kesi ya ubakaji
Bien wa Sauti sol atangaza kupiga chini matumizi ya mitandao ya kijamii