Rapa wa Marekani, Kanye West ametangaza kugombea urais wa Marekani na kuchuana na Rais Donald Trump na aliyekuwa Makamu wa Rais, Joe Biden.

Kanye West ambaye alikuwa akimuunga mkono Trump na kumtembelea Ikulu akiwa na mkewe Kim Kardashian, amesema kuwa huu ni muda wa kuwa na maono mapya ya 2020 ambayo yanahusu kumtegemea Mwenyezi Mungu.

“Ni lazima tuwekeze katika kutimiza ahadi za marekani kwa kumuamini Mungu, kuunganisha maono na kujenga maisha yetu mapya ya siku za usoni. Nitagombea urais wa Marekani,” Kanye West ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, usiku wa kuamkia leo.

Hata hivyo, bado haijafahamika moja kwa moja kama ameshaanza kuchukua hatua za kujaza fomu maalum kwa ajili ya kushiriki uchaguzi huo utakaofanyika Novemba 3, 2020.

Hata hivyo, bado baadhi ya majimbo hayajafika ukomo wa siku ya kuchukua fomu na kuwasilisha ili mhusika aweze kuwa katika karatasi ya kupigiwa kura.

Muigizaji nguli wa kike afariki kwa corona

IGP Sirro ahimiza usajili kampuni binafsi za ulinzi kwenye PSGP, aeleza faida

Simba Queens uso kwa macho na JKT Queens
Muigizaji nguli wa kike afariki kwa corona