Rapa Kanye West wa nchini Marekani amefuta akaunti zake za Twitter na zile za Instagram kwa sababu ambazo hazijajulikani.

Kanye West ameanza kutoweka na kuishi maisha ya ukimya katika mitandao ya kijamii mapema mwaka huu huku mashabiki wake wakimsihi mkewe Kim Kardashian ambaye ni nyota wa Raality TV amwambie mumewe arudi katika mitandao.

Kabla ya kufuta akaunti zake, Kanye West alidaiwa kufuta ujumbe wake uliokuwa ukimuunga mkono Rais wa Marekani, Donald Trump.Hii inatajwa kuwa ni baada ya mkewe kuibiwa vito vyenye thamani ya dola milioni 10.5 mjini Paris mwezi Oktoba.

Hata hivyo, Kardashian amesalia katika mtandao wa Twitter na ana wafuasi milioni 51.

Video: Gwajima Amvaa Nabii aliyetabiri kuhusu hatma ya Uhai wa Lowassa
Dkt. Nchimbi atoa agizo kwa mkurugenzi wilaya ya Singida mjini