Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Marekani Kanye West amesema kuwa utumwa wa Wamarekani weusi uliofanyika zaidi ya miaka 100 iliyopita lilikuwa chaguo lao kwani haiwezekani watu wakakubali kutawaliwa kwa miaka zaidi ya 400 bila kufanya chochote.

 

”Unaposikia kwamba utumwa ulifanyika kwa zaidi ya miaka 400.. miaka 400? ni kama walipendelea hilo kufanyika’,.

Amesema hayo pindi alipofanya mahojiano katika kipindi cha burudani cha TMZ .

Kauli hiyo imeibua hisia za watu wengi akiwemo Bwana Lathan ambaye amesema kuwa matamshi ya msanii huyo yalionekana kutolewa bila kufikiria.

“Una haki ya kuamini chochote unachotaka , lakini ujue kuna ukweli katika dunia ya sasa na athari zake kwa kila kitu ulichosema’, aliongezea huku nyota huyo akisimama na kujikuna kidevu.

“Lazima tukabiliane na ukandamizaji uliotokana na mika 400 ya utumwa ambayo ulisema kuwa watu wetu walipendelea, bwana Lathan aliendelea akiongezea kwamba nimeshangazwa na ndugu yangu nimeumizwa kwa wewe kusema kitu ambacho sio cha kweli.

Katika mahojiano hayo ya TMZ West amemtaja Rais, Trump kuwa rafiki yake na kusema kuwa rais huyo ni miongoni mwa watu wake anaowapenda sana.

Matamshi yake yalizua hisia kali katika mitandao ya kijamii huku watumiaji wa mtandao wa twitter wakisema kuwa msanii huyo anafaa kusoma upya vitabu vya historia.

 

 

Video: Ngorongoro Heroes yaingia kambini
Msigwa anena makubwa kuhusu ongezeko la mishahara