Rapa Kanye West ametishia kuzitosa tuzo za Grammy za mwaka 2017, endapo waandaaji hawatamuingiza Frank Ocean kwenye orodha ya vipengele vya tuzo hizo.

Kanye alitema cheche akiwa jukwaani huko Oakland, California nchini Marekani, ambapo alizipigia debe album mbili za Frank Ocean za Blonde na Endless ambazo licha ya kuwa kubwa hakuna dalili za kuzijumuisha kwenye tuzo hizo za muziki zinazotajwa kuwa kubwa zaidi.

“Album ninayoisikiliza sana mwaka huu ni ya Frank Ocean. Nitawaambia hili sasa hivi, kama album yake haitawekwa kwenye vipengele vinavyoshindaniwa, sitaonekana kwenye Grammy,” Kanye West alifunguka. ”Kama wasanii inabidi tuungane kupambana na upuuzi,” aliongeza.

Kanye West anakumbukwa kwa tukio lake la kumpokonya Tailor Swift tuzo jukwani, baada ya kukabidhiwa tuzo ya Video Bora ya Mwanamuziki wa Kike ya MTV Video Music Awards (MTV VMAs 2009) akidai tuzo hiyo alipaswa kuipata Beyonce.

Video: Waziri Mwijage asema watanzania wanapenda elimu 'mserereko', Azungumzia elimu yake
Afungwa jela miaka 1,503 kwa kumbaka mwanae miaka minne