Msanii maarufu wa nchini Marekani Kanye West amefichua kwamba Jay-Z ni miongoni mwa wasanii walioshiriki katika albamu yake mpya alioizindua Donda- na aliyoipa jina la marehemu mama yeke katika uwanja wa Mercedes Benz , mjini Atlanta katika jimbo la Georgia.

Kanye west aliingia katika ukumbi ambapo albamu ilanza kuchezwa bila msanii huyo kusema neno, na wimbo wa mwisho katika albamu hiyo ilisikika sauti ya Jay Z, rafiki yake wa siku nyingi , mpinzani na mshirika wake.

Mstari mmoja wa msanii Jay-Z ulishirikisha neno ‘’red cap’’ – akimaanisha kofia ya Kanye West ilioandikwa MAGA {‘Make America Great Again’}.

Young Guru, mzalishaji wa muziki na muhandisi ambaye amefanya kazi na Jay-Z , alisema kwamba mstari huo uliongezwa dakika za mwisho.

Ukamataji na faini za kupaki zamkera RC Makalla
Moto wateketeza watoto wa familia moja