Beki wa kulia wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Shomari Salum Kapombe ameanza mazoezi, baada ya kuujuza jeraha ya kifundo cha mguu kwa majuma mawili.

Kapombe alipatwa na majeraha ya kifundo cha mguu wakati wa Mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo Simba SC walisafiri hadi mkoani Mara kucheza dhidi ya Biashara United na kuambulia matokeo ya 0-0.

Beki huyo ameonekana mapema hii leo akiwa kwenye mzoezi ya kikosi cha Simba SC, kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hatua ya kwanza dhidi ya Jwaneng galaxy, utakaochezwa Botswana mwishoni mwa juma hili.

Mwingine aliyeonekana akifanya mazoezi mapema hii leo ni mchezaji kiraka Erasto Nyoni, ambaye pia alikua majeruhi kwa siku kadhaa zilizopita, hali iliyopelekea aondolewe kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichepambana dhidi ya Benin iliyochezwa Dar es salaam na kisha Cotonou.

Kwa upande mwingine kiungo Mzamiru Yassin naye pia amejumuika kwenye kikosi kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes katika mazoezi yaliyofanyika Uwanja wa Boko Veteran, Bunju.

Makambo: Tutatwaa ubingwa 2021/22
Ulega: Mchezo wa Bao uendelezwe ili kumuenzi Baba wa Taifa