Golikipa mkongwe hapa nchini ambaye kwa sasa anachezea Kagera Sugar, Juma Kaseja amepanga kuwa mtangazaji wa radio au televisheni baada ya kustaafu kucheza soka.
 
Ameyasema hayo wakati akihojiwa na kituo kimoja cha radio jijini Dar es salaam, amesema kuwa atakapostaafu kucheza soka ataingia rasmi katika tasnia ya utangazaji, ambapo awali ataanza kwa kutumia kipaji chake lakini kadri siku zinavyozidi kwenda itabidi aingie shule ili kuwa mtangaji mzuri zaidi na bora.
 
“Kila kitu kinahitaji elimu, ila mimi kwanza nitaanza hivi hivi nilivyo halafu kadri nitakavyozidi kwenda nitakuwa najiendeleza na shule ili niwe mtangazaji mzuri” amesema Kaseja
 
Hata hivyo, Kaseja ameongeza kuwa wachezaji wadogo wanaochipukia kwenye soka wanapaswa kuwa wavumilivu, wasikivu kwa walimu wao na kuwa na nidhamu kama wanapokuwa kwa wazazi wao
Watu 19 wafariki dunia ajali ya basi
Bendera aitaka TADB kuwekeza mkoani Manyara

Comments

comments