Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela pamoja na viongozi wengine wa wilaya ya Iringa wamefanya kazi ya kubwa ya kuokoa mwili wa mchimbaji madini katika mgodi wa Nyakavangala, Vaspa Nyenza mkazi wa Itengulinyi Kata ya Ifunda wilaya ya Iringa kwa takribani masaa kumi na nane.

Kasesela amesema kazi ya uokoaji ilianza saa mbili asubuhi alipowasili katika mgodi huyo wa Nyakavangala ambapo walijitahidi kuokoa mwili wa marehemu hadi majira ya saa sita usiku zoezi hilo lilikuwa likiendelea

“Hadi saizi tumepiga dua zote lakini hali ngumu sijui nini kinaendelea katika hili shimo maana waokoaji kila wakiukaribia mwili wa marehemu miamba laini inavungika na kujaza udongo ndani ya shimo ndio maana mmeniona naangaika na ndugu wa marehemu kujaribu kusali huku na kule lakini hali ni ngumu hadi muda huu wa saa tano usiku” – amesema Kasesela

Kasesela amewataka ndugu wa marehemu pamoja na wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi cha majonzi, pia amewataka wachimbaji wengine kuwa makini wakati wa uchimbaji wa madini la sivyo mgodi huo utafungwa.

Akizungumzia tukio hilo, Thomas Masuka ambaye ndiyo mmiliki wa mgodi huo amemshukuru Mkuu wa Wilaya, Richard Kasesela kwa jitihada zake za kuhakikisha shughuli za kuuokoa mwili wa marehemu zinakamirika.

Aidha amesema kuwa atalipa gharama zote kuanzia uokoaji na kuusafirisha mwili nitazilipa mimi kama mmiliki wa mgodi huo kwa mujibu wa sheria za madini.

“Hata angekuwa Mwananchi wa Kigoma, Mwanza, Mbeya, Bukoba na sehemu yoyote ile ndani ya Tanzania basi ni wajibu wangu kuhakikisha mwili wa marehemu unafika mali pake kwa usalama unaotakiwa” amesema Masuka

 

Uli Stielike Atupiwa Virago
Alvaro Morata Anukia Old Trafford