Serikali nchini Kenya, imewasimamisha kazi maofisa 27 kutoka taasisi kumi na mbili wanaotuhumiwa kuachia sukari ambayo muda wake wa matumizi ulikuwa umekwisha na  ilikuwa imepangwa kuharibiwa mwaka wa 2018. 

Mkuu wa Utumishi wa Umma, Felix Koskei alisema kusimamishwa kazi kwa maofisa hao kunatoa nafasi ya kufanyika kwa uchunguzi kuhusu suala hilo ambalo limezua ghadhabu kutoka kwa raia nchini humo. 

Wizara zinazokabiliwa na sakata hilo ni pamoja na ile ya Hazina ya Kitaifa inayoongozwa na Njuguna Ndung’u na Uwekezaji na Biashara inayoongozwa na Waziri Moses Kuria huku Shirika la ukadiriaji wa  ubora wa bidhaa nchini Kenya – KEBS, lilionya kuwa mifuko 20,000 ya sukari haifai kwa matumizi ya binadamu. 

Hatua hiyo sasa imezua hofu miongoni mwa jamii kuwa huenda ikaleta athari kwa afya ya mamilioni ya raia katika taifa hilo la Afrika Mashariki, ambalo linadhaniwa huenda lilinunua sukari hiyo kwa matumizi ya binadamu.

Mabalozi washiriki uletaji Watalii nchini - Mchengerwa
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Mei 19, 2023