Moja ya mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya kipindi kifupi cha serikali ya Awamu ya sita ni shughulikia hoja kumi na moja za Muungano pamoja na kazi kubwa inayoendelea ya kumalizia Hoja 7 za Muungano zilizobaki.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo leo tarehe 05 Oktoba, 2021 alipofanya ziara maalumu ya kumtembelea Dkt. Hussein Mwinyi Ikulu Zanzibar.

Jambo lingine lililowasilishwa na Waziri Jafo ni suala la Chuo cha Serikali za Mitaa cha Hombolo kilichopo Jijini Dodoma kuweza kufungua tawi visiwani Zanzibar ili kuwawezesha Watendaji, Wanafunzi na Madiwani kupata fursa ya mafunzo yaliyobobea katika uendeshaji wa Serikali za Mitaa.

Aidha, Jafo amewashukuru na kuwapongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi kwa imani yao juu yake na kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuimarisha Muungano na kuwaletea maendeleo wananchi wa pande zote mbili za Muungano.

Kwa upande wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi amempongeza Waziri Jafo na Dkt. Khalid Salumu Mohammed, Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Zanzibar kwa ushirikiano wao mkubwa na kuchapakazi kwa kasi na kuwezesha kuondoa hoja 11 za Muungano kati ya hoja 18 zilizokuwa bado hazijapata ufumbuzi hapo awali.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri Mwenyeji Dkt. Khalid Mohammed – Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza wa Wawakilishi, Bi. Mary Maganga Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais-SMT, Bw. Mohammed Abdullah, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais – SMT, na Kaimu Mkurugenzi wa Muungano Bi. Cesilia Nkwamu.

Tanzania kuendelea kunufaika na Shirika la Miliki Ubunifu Duniani
Gari lililozama Baharini Polisi wazungumza