Usiku wa kuamkia leo uongozi wa klabu ya Leicester City ulikuwa na kazi kuwatunuku tuzo wachezaji wao waliofanya vizuri kwa msimu wa mwaka 2016/17, katika hafla iliyofanyika King Power Stadium.

Katika hafla hiyo imeshuhudiwa Mlinda Mlango Kasper Schmeichel akiibuka kidedea baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo mbili za mchezaji bora wa msimu chaguo la klabu na mashabiki baada ya kupata kura zaidi ya asilimia 75 zilizopigwa kupitia mitandao.

Schmeichel mwenye umri wa miaka 30, ametwaa tuzo hizo baada ya msimu huu kuonyesha kiwango bora kilichoisaidia Leceister City kufika robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Ulaya.

Katika michuano hiyo alifungwa mabao matatu tu katika michezo minane huku katika michezo minne ya kwanza akicheza bila kuruhusu bao.

Tuzo ya mchezaji bora chipukizi imekwenda kwa Mnigeria, Wilfred Ndidi wakati tuzo ya bao bora la msimu ikienda kwa kiungo wa England Danny Drinkwater.

Tuzo ya mchezaji bora wa kituo cha kulea na kukuza vipaji kwa vijana (Academy), imekwenda kwa mlinzi, Alex Pascanu ambaye amekuwa muhimili mkubwa kwenye vikosi vya U-18 na U-23 vya klabu hiyo.

Harvey Barnes ametwaa tuzo ya mchezaji aliyeonyesha mafanikio maarufu kama Development Squad Player of the Season Award.

Arsenal Yaanza Mapema Ujenzi Mpya wa Ukuta
Video: Inahuzunisha! Mtoto aliyetaka kuozeshwa na baba yake asimulia mazito