Aliyewahi kuwa Katibu wa Uenezi wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA), Edward Simbeye leo Februari 26, 2020, amejivua uanachama ndani ya chama hicho na kusema kuwa atapumzika siasa kwa muda ili aweze kutafakari kwa kina chama chenye malengo ya kweli.

Amesema ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kuona chama hicho kimetoka kwenye msingi wa kuchukua dola na kimekuwa chama cha watu wachache.

“Moja ya malengo ya chama chochote duniani ni kuchukua dola, Chadema chama changu kimetoka kwenye malengo ya msingi ya kuchukua dola na badala yake kimekuwa chama ama kikundi cha watu wachache. badala ya kuwa chama cha siasa inakuwa kampuni ya mtu binafsi” Amesema Simbeye.

Simbeye ametupia lawama uongozi wa chama hicho kwa kushindwa kutafakari sababu zinazowafanya viongozi kukihama na kuendelea kuwadanganya watu kuwa kipo imara.

” Ukweli ni kwamba watanzania wenzangu chadema haipo imara, tunadanganyana na kunasababu za msingi ambazo tumezificha…Nafikiri huu ndiyo mwisho wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema”.

Simbeye amejivua gamba ikiwa zimepita siku chache tangu aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt. Vicent Mashinji kutangaza kuhamia chama tawala CCM.

Ameeleza kusikitishwa na chama hicho kushindwa kuchukua uongozi katika vijiji hapa nchini kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba mwaka jana jambo ambalo anaona ni taswira hasi kwa uchaguzi mkuu ujao.

Amesema “kwa sasa sioni ‘future’ ya chadema kuwa chama mbadala cha CCM kwa kuwa mwaka 2014 chadema ilishinda zaidi ya vijiji 1000 na sasa tunaelekea uchaguzi mkuu chadema haina kijiji hata kimoja”

Aidha ameongelea idadi ya wabunge ambao wamehama chama hicho licha ya kuwa kubwa, bado kuna ambao anatarajia watahama pia kwa sababu ya chama kupoteza malengo.

“sasa hivi wabunge 11 wameondoka kwenye chama na sio hao tu wabunge wengi wataondoka kwakuwa chama kimepoteza malengo ya kuchukua dola” amesema Simbeye

Aidha amesema Edward Lowasa na Sumaye walikuwa na mchango mkubwa akatika chama hicho lakini walifukuzwa kwa kuwa waliingilia maslahi ya watu binafsi.

Katibu Chadema Manyoni auawa, mwili waokotwa barabarani
Balozi Mongela: Ni hasara kuwa na wanawake viongozi wenye aibu