Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ametunukiwa uraia wa heshima wa Hiroshima nchini Japan, baada ya kuhudhuria sherehe za kuadhimisha miaka 77 ya shambulio la mbomu la nyuklia la Hiroshima lilosababisha maafa ambayo athari zake zinaendelea hadi leo.

Akiwa katika maadhimisho hayo, Katibu Mkuu huyo pia alishiriki katika mambo mbalimbali ikiwemo kuhudhuria mazungumzo na vijana, mkutano na waandishi wa habari na kikao cha pamoja baina yake na Viongozi mbalimbali.

“Ninakubali heshima hii kubwa kwa niaba ya watu wote wa Umoja wa Mataifa ambao wanafanya kazi kwa ajili ya amani duniani, na pia kwa niaba ya wanadiplomasia na wapatanishi watakaokutana jijini New York, Marekani kuzuia kuenea kwa silaha za nyuklia,” ameshukuru Guterres.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres (Katikati), akiwa ziarani nchini Japan. (picha na UN/Ichiro Mae).

Katika ushiriki wake wa mazungumzo yasiyo rasmi na wanaharakati vijana wa Kijapani wanaoongoza mipango ya uondoaji wa silaha za nyuklia, Geterres amesema mbali na mambo mengine muhimu pia Dunia inatakiwa kuwa macho na masuala ya kimataifa.

Antonio Guterres, pia amezungumzia kuhusu hali ya sasa ya dunia, ikiwa ni pamoja na mzozo wa sayari tatu, ukosefu wa usawa unaoendelea, na kuenea kwa vita vya silaha akidai amaji ni muhimu kuliko jambo lolote na kwamba viongozi wa Mataifa wanapaswa kulitambua jambo hili.

Bodaboda kuwasafirisha Wazee, Wagonjwa vituo vya kura
Rais asifia mafanikio ya Jeshi la Ukraine