Katibu tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega amefariki katika ajali ya gari leo Jumatano Februari 3, 2021 wakati akitoka mkoani humo kwenda Dodoma baada ya gari alilokuwa amepanda kugongana na basi.

Akizungumza na Waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joseph Mkirikiti amesema ajali hiyo imetokea eneo la Mdori Mizani.

Amesema katika ajali hiyo watu wengine wanne wamejeruhiwa ambao ni dereva wa katibu tawala huyo na wanawake watatu waliokuwa kwenye basi.

“Ni ajali mbaya kumpoteza Katibu Tawala,” amesema Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Majaliwa: Ondokeni mara moja
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Februari 4, 2021