Katibu wa CCM tawi Kata ya Daraja mbili, Aron Sanare Kivuyo (56) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumbaka na kumpatia ujauzito Mwanafunzi wa Kituo cha Compassion mwenye miaka 15.

Diwani wa Kata ya Daraja mbili, Prosper Msofe amethibitisha kukamatwa na kushikiliwa kwa kiongozi huyo na kueleza wao kama Viongozi wanalaani vitendo vya ubakaji na kuisihi Polisi kufanya uchunguzi ili kubaini ukweli

Mtuhumiwa anadaiwa kumpachika ujauzito Mwanafunzi huyo baada ya kumrubuni kwa kumpatia fedha na mahitaji mbalimbali na baadae alimwomba fadhila ya ngono, jambo ambalo alifanikisha adhima yake.

“Nimegundua kuwa mtoto ana ujauzito kutoka kwa wadhamini wake wanaomsomesha hapo Compassion, mimi kama mzazi wake mlezi nimesikitishwa sana ukizingatia aliyempa huo ujauzito ni kama babu yake”amesema baba mlezi Boniface Mbwambo

Naye mratibu wa kituo hicho, Yona Kaaya amesema walimtilia shaka mwanafunzi huyo kutokana na mabadiliko ya kiafya na alipelekwa kupimwa ujauzito katika hospital ya Mount Meru na kugundulika kuwa ana ujauzito na kumtaja Katibu huyo wa CCM kuwa ndiye mhusika.

Utaratibu mpya kumpata Miss Tanzania watangazwa
Rugemarila aruhusiwa kuwasilisha hoja za kuachiwa huru