Katibu Muenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo jijini Arusha wilaya ya Arusha Mjini, Gabriel Lucas Kivuyo ametangaza kujivua nafasi zote ndani ya Chama hicho na kujiunga na CCM.

Amesema kwa moyo wake mkunjufu ameamua kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika juhudi za kuliletea maendeleo taifa.

Amesema kwasasa kubaki Chadema ni kupoteza muda kwani, Rais Dkt. Magufuli anatekeleza mahitaji ya Watanzania hivyo hakuna haja ya kupinga maendeleo.

Hata hivyo, Katibu huyo amepokelewa na Katibu wa (CCM) Wilaya ya Arusha Mjini, Mussa Matoroka na kusema kwamba chama hicho kina azma ya kuleta Maendeleo.

 

 

Wavamizi wasaka dhahabu kwenye shamba la mke wa Mugabe
Bomberdier Q400 iliyokuwa imezuiliwa Canada kuwasili nchini

Comments

comments