Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila, ana siri kubwa juu ya kufanya vibaya kwa timu yao na amesema kwa sasa anawaanda kisaikolojia na utulivu wachezaji wake, ili kutafuta pointi tatu katika mchezo wao wa mwisho wa kumalizia Mchaka Mchaka wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/20.

Katwila amesema hawezi kuweka wazi matatizo ya timu yake kwa sasa anapigania kutafuta alama tatu muhimu muhimu katika mechi yao dhidi ya Ruvu Shooting.

Amesema baada ya ligi kumalizika ataweka wazi sababu ya wao kutofanya vizuri hali inayosababisha kupambana kujinasua katika nafasi mbaya waliyokuwapo.

“Kwa sasa siwezi kusema chochote sababu tuna mechi moja tunahitaji kupambana kutafuta alama tatu muhimu, sasa nawaandaa wachezaji wangu saikolojia na kuwa watulivu ili tupate alama hizo tujiweke katika nafasi nzuri,” alisema Katwila.

Amesema bila ya kuwajenga kisaikolojia na utulivu wachezaji wake watakuwa na wakati mgumu katika mechi yao ya mwisho.

Katwila amesema ana imani ya kupata matokeo katika mechi yao dhidi ya Ruvu Shooting kwa kujikusanyia alama tatu muhimu na kuiweka timu hiyo katika nafasi nzuri.

“Huu mchezo ni muhimu sana kwetu tunahitaji utulivu wa hali ya juu kupata alma tatu na kujiweka katika nafasi nzuri, suala la kushuka daraja haliwezekani tunaenda kupambana,” alisema Katwila.

Hata hivyo baada ya mchezo dhidi ya Young Africans uliochezwa Julai 22 Mjini Morogoro Uwanja wa Jamuhuri na kushuhudia Mtibwa Sugar wakibanwa kwa matokeo ya sare ya bao moja kwa moja, Katwila alisema hajafurahishwa na mwenendo wa timu yake msimu huu na matokeo iliyoyapata hivyo anaweza kujiuzulu.

“Nipo tayari kujiuzulu kwa sababu ya matokeo mabaya, kama kocha ninatakiwa kuiongoza timu kushinda,” alisema Katwila ambaye  ameweka rekodi ya kuibebesha Mtibwa Kombe la Mapinduzi akiwa mchezaji na baadaye kocha.

Mtibwa Sugar inahitaji alama tatu tu, ili ijikusanyie jumla ya alama 45 ambayo kwa sasa ipo nafasi ya 14 ikiwa na alama 42 wakia chini ya Mwadui FC wenye alama 44 wakiwa nafasi ya 13, huku KMC wakiwa na alama 46 katika nafasi ya 12 kwenye msimamo msimamo wa Ligi Kuu.

Wakati Mtibwa Sugar wakijipanga kumaliz Mchaka Mchaka wa Ligi kuu Msimu huu 2019/20, michezo mingine ya kufunga pazia la msimu huo itakayochezwa mwishoni mwa juma hili itakua kama ifuatavyo,

Alliance FC vs Namungo FC (Nyamagana -Mwanza)

 Mbao FC vs Ndanda FC (CCM Kirumba -Mwanza)

KMC FC  Vs Mbeya City FC (Azam Complex -Dar es Salaam)

Singida United vs  Biashara United (Liti -Singida)

Mwadui FC vs Kagera Sugar (Mwadui Complex -Shinyanga)

Polisi Tanzania vs Simba SC (Ushirika -Moshi)

Coastal Union vs Jkt Tanzania (Mkwakwani -Tanga)

Mtibwa Sugar  vs Ruvu Shooting (CCM Gailo -Morogoro)

Tanzania Prisons  vs Azam FC (Sokoine -Mbeya)

Lipuli FC vs Young Africans (Samora -Iringa)

Odinga: Namkumbuka Mkapa usuluhishi uchaguzi 2008
Nenda Mzee Mkapa ila kwa hili umetuheshimisha na hatutokusahau