Msanii wa Marekani Catheryn Elizabeth Hudson maarufu kama Katy Perry amekuwa mtu wa kwanza duniani kupata wafuasi milioni 100 katika mtandao wa Twitter.

Msanii huyo aliyezaliwa tarehe 25 Octoba mwaka 1984 ameweka rekodi hiyo huku akifuatiwa na mwimbaji kutoka Canada Justin Bieber mwenye wafuasi milioni 96.7 wakati rais mstaafu wa Marekani Barack Obama akishika nafasi ya tatu kwa kuwa na wafuasi milioni 91.

Mtandao wa twitter umechapisha kanda ya video inayoonyesha jumbe zake zote tangu alipojiunga na mtandao huo pamoja na ujumbe unaosema “Today, we #WITNESS history” akimanisha”leo tumeshuhudia historia”

 

Vigogo wa IPTL wapandishwa kizimbani
Azarenka kupambana na Risa Ozaki

Comments

comments