Kauli ya machifu kudai kuwa hautambui mamlaka imesababisha kuzuka kwa mapigano ya kugombania ardhi na watu 13 kuuawa na wengine 40 kujeruhiwa huko Las Anod, mji ambao unagombaniwa na vikosi vya Somaliland na Somalia.

Mapigano hayo, yalianza hapo alfajiri ya Februari 6, 2023 kati ya vikosi vya serikali vilivyoko karibu na mji huo na wapiganaji wa ndani, ikiwa ni siku moja baada ya tangazo la machifu wa kimila kudai hawaitambui mamlaka ya Somaliland.

Mapigano katikati ya mitaa uraiani. Picha ya CNN.

Mji huo wa Las Anod, unakabiliwa na mzozo kwa miaka mingi kati ya jimbo lililojitangaza kujitawala, ambalo lipo upande wa kaskazini, na jimbo la Somalia la Puntland, lililopo eneo la kusini.

Inaarifiwa kuwa, takriban watu 20 waliuawa, katika eneo lililojitenga la Somalia mwanzoni mwa mwezi Januari 2023 huko Somaliland, katika mapigano kati ya waandamanaji wanaoipinga serikali na vikosi vya usalama.

Wizara imekusanya zaidi ya bil. 90: Dkt. Mabula
Kamati TPLB yatengua maamuzi