Hebu nikupitishe kidogo kwenye mitaa ya udaku… Dunia ya mtandaoni hususan makazi ya ‘udaku’ imewaka moto wa vita kuu ya maneno na michambo kati ya Malkia wawili wa Instagram,  Zari The Boss Lady na Mange Kimambi uliowashwa na njiti ya kiberiti cha sentensi chache za Diamond Platinumz.

Ni kama kauli ya Diamond aliyoitoa alipofanya mahojiano na Wasafi FM kuhusu nyumba yake anayokaa Zari na wanaye wawili nchini Afrika Kusini imegeuka kuwa silaha kuu ya Mange dhidi ya mrembo huyo wa Uganda.

Diamond alisema kuwa ingawa hana maelewano mazuri na Zari kuhusu malezi ya watoto, hajaamua kumuondoa kwenye nyumba hiyo na kwamba angeweza kufanya hivyo hata kwa kuiuza ‘juu kwa juu’ kwa sababu yeye ndiye ana nyaraka zote.

Hatua hiyo imemuibua Mange ambaye amemsakama Zari akihoji kuhusu tambo za utajiri wa majumba na magari aliyonayo, akidai kuwa kama kweli ana majumba hapaswi kuendelea kukaa kwenye nyumba ya Diamond huku anapewa kauli za vitisho vya kuondolewa muda wowote.

Leo, Zari ameamua kumjibu Mange kupitia kipande cha video ambapo amemtaka kuachana na maisha yake huku akimhakikishia kuwa ana majumba mengi ambayo atamuonesha hivi karibuni. Kitu cha msingi, Zari aliamua kutumia lugha yetu ya Taifa kufikisha ujumbe wake kwa mara ya kwanza kwa ufasaha, huenda ni kutokana na hisia kali za kuumizwa na kauli za hasimu wake huyo.

“Sikiliza wewe bibi kigalula wa UK, hapo huyo kibabu wako hawezi hata kukununulia PK (jojo). Mwenzako nanunuliwa maua, naletewa pesa, nanunuliwa kila kitu mpaka magari ninayo naendesha, mambo ya nyumba isikupe kichwa, nyumba ninazo za Ivan (marehemu), nyumba ya kaka yako tu inakuuma mpaka *****,” alisema Zari kwenye video, kilichofuata ni matusi ya nguoni.

Mange alijibu kwa urefu zaidi lakini msingi wa ujumbe wake ni, “leo nimekushika, yaani hadi umejirekodi unatukana Kiswahili, hujawahi kwenye maisha yako, nimekupatia nimekuminya palepale… umepatikana.” Mengine ni matusi.

Wawili hao wamejibizana kwa lugha kali zenye matusi ya nguoni, huku wote wakijiweka kwenye mstari wa kupambana na kauli ya Diamond na nyumba yake ya Afrika Kusini.

Zidane avunja ukimya kuhusu kuwanyakua Hazard, Neymar
Vurugu zazuka kanisani baada ya Bwana Harusi kudaiwa ni mume wa mtu

Comments

comments