Mbunge wa Jimbo la Sengerema Hamis Tabasamu, amewataka vijana kusoma na kuhakikisha wanajielimisha wenyewe kwa kuwa na uwezo wa kujiajiri na siyo kutegemea ajira serikalini kwani serikali haina ajira.

Kauli ya mbunge wa Sengerema imeibua minong’ono miongoni mwa vijana waliohudhuria mkutano wa Rais Samia mkoani Mwanza.

Tabasamu amewahimiza vijana waliofika katika mkutano huo wanaosoma katika shule za sekondari na vyuo kusoma kwa bidii wakilenga kutumia elimu na ujuzi waliyoupata kujiajiri.

Itakumbukwa siku chache zilizopita Mbunge huyo alinukuliwa Bungeni akilalamika kutishiwa maisha, kauli hiyo aliyoitoa iligusa hisia za vijana waliohudhuria kwa kuwa ilisikika minong’ono  lakini mbunge huyo aliendelea kuzungumza.

“Vijana someni na wekeni katika akili yenu na someni mkitambua kwamba tunasoma tuelimike, na tukielimika tujiajiri wenyewe ajira serikalini hakuna,” amesema Mbunge Tabasamu.

Wasanii kuanza kulipwa kuanzia Disemba
Mwanafunzi wa kidato cha 3 amuua baba yake kwa kipigo kisa ‘kuku’