Katika mazungumzo yaliyafanyika leo, Dk Slaa amefafanua kuwa yeye bado ni mwanachama halali wa Chadema na CCM kwa mujibu wa Sheria kwani anadai kuwa hakuwahi kurudisha kadi za vyama hivyo.

”Sikurudisha kadi ya CCM wala Chadema, sheria inasema uanachama unajulikana kwa kadi na pia kuonekana kwenye jukwaa la chama au vinginevyo si mwanachama” amesema Dk Slaa.

Ameongezea kuwa anasikitishwa kuona upinzani nchini hauna sera zilizonyooka.

”Nasikitika kwa sababu nilishirika kujenga upinzani nchini na sioni chama chenye sera zilizonyooka” amesema Dk slaa.

Aidha kupitia mahojiano hayo Dk. Wilbard Slaa ameeleza  nia na madhumuni ya kurejea nchini na kusema kuwa amerejea kwa lengo la kushughulikia usajili wa Hospitali ya CCBRT, na kutujulisha kuwa yeye ni mwenyekiti wa hospitali hiyo.

Watanzania wengi wamekuwa wakijiuliza maswali juu ya uteuzi wake na kuhoji zoezi zima la uapishwaji na kupangiwa kituo cha kazi, hivyo kwa ujio huu wangi walidhani kuwa amerejea kwa dhumuni la kuaoishwa, La-hasha.

Novemba 23, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanaznia John Pombe Magufuli alimteua, Dk Slaa kuwa balozi ila mpaka sasa bado hajaapishwa na kupangiwa kituo cha kazi.

Seedorf achaguliwa kuwa kocha mpya Deportivo
Kabila kuachia madaraka, ampanga mrithi wake