Mbunge wa Jimbo la Kawe kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee anashikiliwa na jeshi la polisi Kinondoni kwa madai ya uchochezi baada ya kuhojiwa kwa saa mbili na kisha kunyimwa dhamana.

Mbunge huyo alikuwa akiendelea kuhojiwa na mkuu wa upelelezi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni (RCO) kwa kosa la uchochezi.

Aidha, Wakili wa Mbunge huyo, Hekima Mwasipu amesema kuwa Mdee ameitwa polisi kwa kosa la uchochezi ambapo amedai ni kutokana na kauli alizozitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mikocheni Februari 21, 2018.

“Polisi wamemuita kwa kosa la uchochezi kutokana na kauli alizozitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Mikocheni juzi.” amesema Mwasipu.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, siku ya leo, Halima Mdee alitoa taarifa ya kuitwa polisi, kwa kuandika kuwa “Nimepokea wito kituo cha Polisi Oysterbay kwa mahojiano.”

 

Mbunge wa viti maalum CCM Lindi Mjini atoa msaada
Halmashauri zote nchini zatakiwa kutenga 10% ya mapato

Comments

comments