Kocha wa Young Africans Cedric Kaze amemkingia kifua mshambuliaji wake kutoka nchini Ghana Michael Sarpong kwa kusema bado anaimani na mshambuliaji huyo.

Kaze amejitosa kumtetea mshambuliaji huyo kufuatia baadhi ya wadau wa soka nchini kumshambulia Sarpong, kwa kusema ameshuka kiwango na hachezi kama alivyotarajiwa kabla ya kutua Young Africans.

Kaze amesema hana shaka na uwezo wa mshambuliaji huyo aliejiunga na Young Afrika kama mchezaji huru, baada ya kuachana na Rayon Sport ya nchini Rwanda mapema mwaka jana.

Amesema anashangaa kuona wadau wa soka la Bongo wanavyomsakama mshambuliaji wake, japo yeye kama kocha anaridhishwa na uweo wake mazoezini na ndio maana amekua akimpa nafasi ya kucheza michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Watu wanajidangaja sana, mshambuliaji sio kwamba anatakiwa kufunga magoli mengi. Mshambuliaji anaweza kufanya kazi ya kusaidia watu wengine kufunga ndio maana hadi leo nina imani na Sarpong kwa sababu anasaidia wenzake [Kaseke, Tuisila] kufunga,”

“Tunajua anaweza akafunga na itamsaidia kuongeza kujiamini kwenye mechi nyingine.” Amesema Cedric Kaze.

Sarpong ameshaifungia mabao manne Young Africans katika michezo zaidi ya kumi aliyocheza kwenye kikosi cha klabu hiyo kwa msimu huu 2020/21.

Masau Bwire amlaumu Martin Saanya
Wanne washikiliwa tuhuma za uvamizi Bunge la Marekani