Uongozi wa Young Africans umemteua Kocha kutoka nchini Burundi Cedric Kaze kuwa Mkurugenzi wa ufundi wa timu za vijana chini ya miaka 17-20 na timu ya wanawake, Yanga Princess huku akiwa anaendelea na majukumu yake kama kocha msaidizi kwenye timu kubwa.

Kaze amekabidhiwa majukumu hayo wakati huu ambao timu hizo zinajiandaa na msimu mpya wa 2022/23, na zikiwa zimefanyiwa mabadiliko makubwa kwenye vikosi vyao baada ya kuviimarisha kwenye dirisha la usajili.

Lengo kubwa la uongozi wa Young Africans kumpa Kaze jukumu hilo ni kutaka kuwa na falsafa moja kuanzia soka la vijana, wanawake hadi timu kubwa.

Kaze anapewa nafasi hiyo akiwa na uzoefu na soka la vijana ikiwemo timu za Taifa za Burundi kwa vijana wa U-17, U-20, U-23 , timu ya vijana za Barcelona na FC Edmonton za Canada.

Kocha huyu amewahi pia kuwa mchambuzi kwenye kikosi cha vijana cha Ujerumani kilichotwaa ubingwa wa dunia wa chini ya miaka 21 akifanya kazi na wachezaji wakubwa kama Manuel Neuer, Mesut Ozil, Sammie Khedira, Matts Hummels na Toni Kross.

Hans Van Der Pluij: Ninazitaka alama tatu za Young Africans
PPRA yawapa ujumbe Maafisa Maendeleo, Wananchi kuneemeka