Kocha msaidizi wa Young Africans Cedric Kaze ametoa sababu za kufanya maamuzi ya kumtoa Mlinda Lango Aboutwalib Mshery na kuingia Erick Johora katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam FC.

Kaze ametoa sababu hizo kufuatia lawama za baadhi ya Mashabiki na Wanachama wa Young Africans ambao walionesha kuchukizwa na maamuzi hayo, huku wakiamini yalichangia kikosi chao kufungwa kwa changamoto ya Mikwaju ya Penati.

Kaze amesema maamuzi aliyoyachukua yalikua ya kawaida, na siku zote yamekua yakifanywa na makocha wengi duniani, na kilichotokea ni sehemu ya matokeo ya mchezo wa soka.

Amesema Mlinda Lango Johora amekua akifanya vizuri kwenye mazoezi hasa uokoaji wa mikwaju ya Penati, hivyo aliamini engeweza kuisaidia Young Africans kwenye mchezo huo, lakini bahati haikuwa kwao.

“Ni mabadiliko ya kawaida tu, Johara alifanya vizuri sana kwenye mazoezi, tulifanya mazoezi ya penalti na akaonekana kuwa vizuri ndio msingi wa mabadiliko yale,” amesema Kaze.

Tayari kikosi cha Young Africans kimesharejea jijini Dar es salaam kuendelea na maandalizi ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho ‘ASFC’.

Ahmed Ally: Simba SC inatumia mfumo wake
Makomando wakipita mbele ya Rais: Sherehe za Mapinduzi