Wachezaji wa Young Africans waliosalia kikosini wameanza maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo FC, ambao utachezwa mara baada ya Taifa Stars kumaliza mtihani wa kuikabili Tunisia.

Stars itacheza dhidi ya Tunisia katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa Afrika (AFCON 2021), Novemba 13 mjini Tunis na kisha watarudiana jijini Dar es salaam  November 17.

Kocha mkuu wa Young Africans Cedric Kaze, amesema kuanzia jana wachezaji ambao hawajajiunga na timu zao za taifa, wameanza mazoezi, na kwa upande wake mchezo dhidi ya Simba umeshapita na sasa wanaingia msituni kwa ajili ya maandalizi ya mchezo mwingine wa mzunguuko wa 11.

Amesema miongoni mwa wachezaji walioanza mazoezi ni viungo Haruna Niyonzima na Carlos Carlinhos ambao walikua majeruhi.

Wachezaji hao hawakuwapo katika michezo iliyopita ukiwamo dhidi ya Simba ambayo ilimalizika kwa sare ya bao 1-1 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam Jumamosi Novemba 07.

Kaze amesema kwa sasa wameanza kufanya mazoezi na wanaweza kuwamo katika mipango yake kwenye mechi yao ijayo dhidi ya Namungo FC Novemba 22, mwaka huu, baada ya Kalenda ya FIFA kupita.

“Asante sana wananchi kwa sapoti yenu, jana tulirudi kazini, kujiandaa na mchezo wetu dhidi ya Namungo FC kuhakikisha tunafanya vizuri kwa kutafuta pointi muhimu, ligi imekuwa na ushindani mkubwa, hivyo hatuna muda wa kupoteza tunataka kuhakikisha makosa yaliyojitokeza tunayafanyia kazi mapema,” amesema Kaze.

Wachezaji wa Young Africans ambao wamejiunga na Taifa Stars kwa ajili yamchezi dhidi ya Tunisia ni Metacha Mnata, Bakari Mwamnyeto, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Shaibu Abdallah ‘Ninja’, Farid Mussa na Ditram Nchimbi.

Magori: Fraga ameikwamisha Simba SC
Simba SC yapelekwa Nigeria, Namungo yatupwa Sudani Kusini